Saturday, September 8, 2012

KINDAMBA FAMILY CRISIS CHINI YA UFADHILI WA TBL YASAIDIA VIJIJI VISIMA VYA MAJI 15 WILAYANI LUDEWA


Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo akinywa maji kuashiria kuwa ni safi na salama kwa matumizi ya binadamu katika hafla ya kukabidhi mradi wa visima 15 wilayani Ludewa, Mkoa waNjombe hivi karibuni. Mwenye nguo nyeusi katikati ni Cannon  John Kwetu  mratibu wa mradi ambao ulifadhiliwa na TBL.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto) akimtwisha ndoo ya maji Mkazi wa Ngelenge, Kata ya Manda,wakati wa uzinduzi wa visima 15 vilifadhiwa na TBL, wilayani Ludewa, Mkoa waNjombe hivi karibuni.
Katibu Tarafa wa Ngelenge, Januari Mwambeleko akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa visima 15 vilivyojengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), katika baadhi ya vijiji wilayani Ludewa, Mkoa mpya wa Njombe. Kulia ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo. Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni wilayani humo.
Mwambeleko akipampu amaji kwenye moja ya visima hivyo
Steve Kindo (wa pili kulia) wakwanza kushoto ni mratibu wa mradi huu Cannon John Kwetu akiwa na baadhi ya maofisa wa TBL pamoja na viongozi wa vijiji wilayani Ludewa walionufaika na mradi huo